top of page

ASKOFU MWAKIHABA AZINDUA USHARIKA WA ILEMI JIMBO LA MBEYA MASHARIKI

UZINDUZI WA NYUMBA YA MTUMISHI ILEMI

Mwinj. Ezra E. Mbenanga

26. Sept. 2025

UZINDUZI USHARIKA WA ILEMI

Tarehe 25.09.2025 Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Konde Askofu Geoffrey Samuel Mwakihaba ameongoza mamia ya Wakristo wa Usharika wa Ilemi wa Jimbo la Mbeya Mashariki; katika ibada ya Uzinduzi wa Usharika huo.


Ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Msaidizi wa Askofu Mchg. Dkt. Meshack Njinga pamoja na Viongozi wa Dayosisi ya Konde Wakuu wa Majimbo wa majimbo manne pamoja na Wachungaji wa Jimbo la Mbeya Mashariki.


Pamoja na ibada ya uzinduzi wa Usharika Askofu alizindua na kuweka wakfu nyumba ya kuishi Mtumishi na gari la Usharika.


Katika salaam zake Mwakihaba amewashukuru wakristo kwa kazi kubwa walioyoifanya kwa kipindi kifupi na akitumia salaam hizo kuzikumbusha sharika nyingine ambazo zinatumia majengo na mali nyingine bila ya kuweka wakfu.


Aidha msaidizi wa Askofu katika mahubiri amewataka wakristo kuwa waombaji wa kweli katika maisha yao kwani maombi ya kweli yana nguvu katika kuleta majibu chanya kwao.

bottom of page