
Ev. Ezra Mbenanga
15. Okt. 2025
Ziara ya Kikazi ya viongozi wa KKKT katika Dayosisi ya Konde
KKKT Dayosisi ya Konde leo imetembelewa na ugeni toka Ofisi kuu ya KKKT ambao umeongozwa na Katibu Mkuu, Rogath Mollel, Naibu Katibu Fedha Utawala, Adrian Olotu, Mkurugenzi wa Afya Dr. Mbando, Madaktari na watalam wengine wa fedha toka Ofisi hiyo. Lengo ya ziara ni kuangalia mifumo yetu ya uendeshaji katika Hospital zetu. Kuona pia uendeshaji wa idara mbali mbali za udaktari na usimamizi wa fedha.
Ofisi ya Katibu Mkuu DKO ikiongzozwa na Katibu Mkuu Adv. Benjamin Mbembela uliupeleka uongozi huo toka KKKT kutembelea ujenzi Ofisi kuu ya Dayosisi ambayo inajengwa Tukuyu na wameipongeza sana Dayosisi ya Konde kwa mradi huo, kipekee wamempongeza Store Keeper Bi. Lidia kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.