
Ev. Ezra Mbenanga
15. Okt. 2025
Wanafunzi 30 wahitimu Kozi zao Matema
Leo tarehe 15 Oktoba, 2025 kumefanyika Mahafali ya 33 ya Chuo cha Biblia na Ufundi Matema chuo hiki kipo Wilayani Kyela na kinamilikiwa na KKKT Dayosisi ya Konde, ambapo kinaendesha mafunzo ya Uinjilisti, Parish Worker pamoja na ufundi stadi.
Katika Mahafali ya leo mgeni Rasmi alikuwa Msaidizi wa Askofu wa KDO ambapo amewataka wahitimu wakamtumikie Mungu kwa namna ambavyo Roho atawaongoza na wasitumie elimu zao vibaya bali wamtangulize Mungu. Na wanapoenda sharikani watambue kuwa wao sio wasaidizi wa Wachungaji bali ni watenda kazi pamoja nao. Pia huduma ya Mungu hahitaji majivuno wala kuweka madaraja katika Utumishi kwani watu wanataka matunda ya elimu yao, hivyo hekima ya Mungu iwaongoze ambayo hiyo itawapa nguvu ya kuwaongoza watu.
Wanfaunzi 27 waliohitimu ni wa ngazi ya Uinjilisti na 3 ni Parish Worker.