top of page

Ugeni wa wachungaji kutoka KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani

picha ya pamoja ya Baba Askofu Geoffrey Mwakihaba na wachungaji kutoka KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Mwj. Ezra Mbenanga

24. Sept. 2025

Ugeni kutoka KKKT-DMP

Leo ofisi ya KKKT DKO imepata nafasi ya kutembelewa na ugeni kutoka KKKT DMP, wachungaji wapatao 35 kutoka jimbo la Kaskazini, ambao wana ziara ya siku 7 katika Dayosisi ya Konde. Katika ziara hiyo watatembelea majimbo ya Mbeya Mashariki na Tukuyu. Ziara hiyo ya kiutumishi ni ya kudumisha mahusiano yaliyopo kati ya majimbo haya mawili na jimbo hilo la Kaskazini KKKT DMP. Wachungaji hao wameongozana na mkuu wao wa Jimbo Mch. Jacob Mwangomola. Pamoja na kutembelea jimbo la Tukuyu, wametembelea ofisi kuu ya KKKT DKO, pia walipata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa ofisi kuu ya KKKT-DKO inayojengwa Tukuyu. Wachungaji hao wamechangia jumla ya TZS 5,000,000/= (Shilingi milioni Tano) Taslim, ili kuunga mkono juhudi kubwa za KKKT DKO katika ujenzi wa ofisi kuu ya Dayosisi. Katika salamu zake Askofu Geoffrey Mwakihaba amewashukuru Wachungaji hao kwa moyo wao wa upendo waliouonyesha kwa kuamua kuja kufanya kazi ya Mungu na kujifunza katika Dayosisi ya Konde. Amewasihi umoja huo uendelee katika kuujenga mwili wa Kristo.

bottom of page