top of page

Ev. Ezra Mbenanga
19 okt. 2025
KURA ZA MAONI ZA WANAKONDE
Leo ni siku muhimu sana kwa Wana KKKT Dayosisi ya Konde ambapo wanakwenda kupiga kura za maoni kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa Dayosisi. Uchaguzi huo ambao unakwenda kufanyika katika sharika zote za Dayosisi utahusisha Wakristo wote kuanzia umri wa miaka 18 waliopata kipaimara.
Kura hizo ni mapendekezo kwa ajili ya viongozi katika ngazi ya Askofu na Msaidizi wa Askofu. Mchakato huo utakapokamilika kura zitakusanywa na kupelekwa Jimboni na baadae majina yatapelekwa Dayosisi na yale machache yatakayokuwa yamepata kura za kutosha yatapelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa XV wa KKKT Dayosisi ya Konde utakaofanyika kuanzia tarehe 13 - 15 Novemba, 2025 katika Usharika wa Kanisa Kuu Tukuyu.
bottom of page