top of page
askofu.jpg

Neno kutoka kwa Askofu

Napenda kuchukua nafasi hii kuwaalika kwa furaha katika tovuti yetu rasmi ya Dayosisi ya Konde, ambapo mtapata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu namna Dayosisi yetu inavyoendelea katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kiroho, elimu, afya, na huduma nyinginezo. KKKT Dayosisi ya Konde imejizatiti katika kuhubiri habari njema za wokovu kupitia YESU KRISTO, na tunajivunia kutekeleza kazi hii kwa ufanisi mkubwa.

Tunayo njozi yenye nguvu inayosema: 'Ushirika wa Kikristo unaotangaza Habari Njema na Kukuza maisha bora kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote'. 

Kauli mbiu yetu inasema: 'Uinjilishaji, uchaji, na ushuhuda mwema.' Huu ni mwongozo wetu katika huduma zetu, tukiwa na lengo la kuwafikia watu wote kwa upendo na kuwapa matumaini ya maisha bora.

Karibuni sana katika tovuti yetu ili muweze kufahamu kwa undani zaidi kuhusu shughuli na mipango ya Dayosisi yetu. Mungu awabariki sana, na awape neema katika kila jambo linalohusiana na huduma ya Kristo.

01.

Kuelekea Mkutano Mkuu wa XV 13-15 No.2025

Uchaguzi mkuu ndani ya KKKT-DKO

02.

KONDE Marathon 2026

Kujiandaa na Konde

Marathon 2026

03.

This Is a Title

Umoja, Amani na mshikamano ndani ya Kanisa

Historia ya DKO

Kanisa kuu KKKT-DKO
Kaburi la wamisionari wa kwanza KKKT-DKO
Jubilee ya Injili, KKKT-DKO

Konde ni moja ya Dayosisi 28 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), iliyoko Nyanda za Juu Kusini katika mikoa ya Mbeya na Songwe, ikiwa na zaidi ya waumini 125,000. Ilianzishwa wakati wa kazi za kimisionari za karne ya 18, ikitoa huduma za kiroho na kijamii. Makao makuu yako Tukuyu, Wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Imeandikishwa tarehe 26 Septemba 2000 chini ya Sheria ya Vyama ya 1954, na inafanya kazi chini ya sheria ya  Na. 375 ya Wadhamini na Sheria ya Uingizaji ya Tanganyika ya 1971, iliyorekebishwa mwaka 2002. Ni mwanachama wa Jumuiya ya  Kikristo la Tanzania (CCT) na inafanya kazi katika mikoa ya Mbeya na Songwe, ikijumuisha wilaya kama Kyela, Rungwe, Jiji la Mbeya, Mbeya Vijijini, Mbozi,Momba, Ileje, na Wilaya ya Songwe (eneo la Ifwenkenya).

Kiutawala, Askofu ndiye Mkuu wa Dayosisi, akisaidiwa na Msaidizi wa Askofu kwa masuala ya kichungaji na Katibu Mkuu kwa kazi za kiutawala. Katibu Mkuu ana manaibu wawili: mmoja wa Fedha, Mipango, na Maendeleo, na mwingine wa Malezi ya Kikristo na Huduma za Kijamii. Wa kwanza anasimamia Idara za Fedha na Mipango na Maendeleo, wakati wa pili anasimamia Idara za Wanawake na Watoto, Huduma za Afya, na Elimu ya Kikristo na Kazi za Vijana.

Kwa sasa Dayosisi ya Konde ina  Majimbo yapatayo 8 na sharika zipatazo 115

Wachungaji, wakiwa katika ibada ya kumsimika Askofu Gofrey Mwakihaba
Mkuu wa mkoa, akisalimiana na viongozi wa kanisa
Kanisa kuu, KKKT-DKO
Konde marathon 2025

Konde Marathon 2025

Matema Lutheran Hospital

Miradi ya Dayosisi

Dhamira ya Dayosisi

Kumhudumia mwanadamu kikamilifu;kiroho, kimwili na kiakili kwa kuwawezesha watu kumjua Yesu Kristo na kuishi maisha yao kwa ukamilifu kulingana na mafundisho ya Biblia,utambulisho wa Kilutheri, na katiba ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  Tanzania Dayosisi ya Konde. 

Dira ya Dayosisi

Ushirika wa Kikristo unaotangaza Habari Njema na Kukuza maisha bora kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote.

Kauli mbiu ya Dayosisi

Uinjilishaji, uchaji na ushuhuda mwema

  • Instagram
  • elct konde tv
  • Threads
bottom of page