KKKT-Dayosisi ya Konde
Dayosisi ya Konde ni mojawapo ya dayosisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), yenye makao yake makuu mjini Tukuyu, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Dayosisi hii ilianzishwa kwa lengo la kueneza injili ya Yesu Kristo pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa watu wa Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mbali na huduma za kiroho, Dayosisi ya Konde imekuwa mstari wa mbele katika kutoa mchango mkubwa katika sekta za elimu, afya, maendeleo ya jamii, pamoja na miradi ya kiuchumi inayosaidia kuinua hali za maisha ya watu.
Konde inaundwa na majimbo kadhaa ambayo yamesambaa katika mikoa ya Mbeya na Songwe. Majimbo haya ni Jimbo la Mbeya Mashariki, Jimbo la Mbeya Magharibi,Jimbo la Magharibi, Jimbo la Tukuyu, Jimbo la Kyela, Jimbo la Kati, pamoja na Jimbo jipya la Kamsamba (Missioni), Jimbo la Mwakaleli. Kila jimbo linaundwa na sharika mbalimbali ambazo ndizo msingi wa huduma za kichungaji na kijamii. Kupitia mfumo huu, dayosisi inasimamia sharika zake, hospitali, vituo vya afya, shule, vyuo vya Biblia na ufundi, pamoja na miradi ya maendeleo inayolenga kuimarisha mshikamano na kuinua maisha ya jamii yote.

Viongozi wa Dayosisi

Mchg. Geofrey mwakihaba
Askofu KKKT-DKO

Mchg. Dkt. Meshack E, Njinga
Msaidizi wa Askofu KKKT-DKO

Adv. Benjamin Mbembela
Katibu Mkuu KKKT-DKO

Kissa Mwamfupe
Naibu katibu Mkuu, Fedha Mipango na Maendeleo

Cesilia Nsobo
Naibu katibu Mkuu, Huduma za Jamii

Dkt. Lee Mwakalinga
Naibu katibu mkuu, Huduma za Afya.